Nyumba kubwa zenye vyumba vingi zinakula umeme mwingi sana. Familia na wageni wanaweza kusahau kuzima baadhi ya swichi za umeme. Pia, vyumba vya chini ya nyumba na vingine kama hivyo vinakula sana umeme hata kama hakuna mtu ndani yake.
Kiujumla, bili ya umeme itaongezeka kutokana na ukubwa wa nyumba yako.
Unaweza kudhibiti yote haya kwa kutumia mfumo wa kisasa wa uangalizi wa nyumba. Lakini, unaweza kuwa unajiuliza, je, ni rahisi kutumia mfumo kama huu? Je, unaweza kuokoa umeme? Je, ni kwa namna gani unaweza kuokoa umeme?
Bidhaa mbalimbali zenye waya na zisizokuwa na waya za kisasa zinapatikana katika soko. Asilimia sabini ya bidhaa hizi zinahitaji binadamu kuwepo na kutoa amri juu ya nini kifanyike, hivyo vifaa hivi haviwezi kuhesabiwa kwamba vina uelevu kama vile vinavyoweza kugundua kuwa sasa kuna haja ya kufanya mabadiliko na kufanya vijiendeshe vyenyewe, bila kuhitaji uwepo wa binadamu ili kufanya kazi. Kwa lugha nyingine, ubora wake unaonekana pale kifaa kinapoamua chenyewe muda muafaka wa kuzima na kuwasha vitu.
Wasambazaji wengine wanaweza kuwa na vifaa vya kisasa zaidi ya vile vya TIS kwa namna moja, lakini vifaa vyao havina uwezo wa kutimiza mahitaji yote ya udhibiti wa kisasa wa ndani ya nyumba. Hivyo, vifaa vyao ni lazima viunganishwe na vile vya makampuni mengine.
Ufungaji wa nyaya kwa ajili ya mfumo wa kujidhibiti wenyewe, haswa kwa vifaa kama motion sensors, infrared emitters, contact sensors, thermostats, na vifaa vingine vinavyotakiwa kuungwa kwenye mfumo wa kati wa uendeshaji, vinahitaji nyaya nyingi sana, muda, pesa ,nguvu kazi pamoja na uwekaji wa programu. Zaidi ya hayo, ufanyaji wake kazi kwa ufanisi wa juu sio jambo linaloweza kuhakikishiwa katika mifumo kama hiyo, jambo ambalo ni la kawaida kwa vifaa vya kisasa.
Kampuni ya TIS Smart Home inaweza kukusaidia kupunguza gharama ya mradi na kukupatia uokoaji wa umeme ulio na ufanisi mkubwa kwa kutumia njia zifuatazo:
Kundi la makampuni ya TIS imefunga vifaa vya udhibiti kwenye zaidi ya villa 300 za kifahari na majumba makubwa huko Mashariki ya Kati. Tunaamini ya kwamba maisha ya kifahari yanaweza kwenda pamoja na uokoaji wa nishati.
Tunatumia kuki kubinafsisha yaliyomo, kubinafsisha na kuchanganua utangazaji na kuhakikisha matumizi salama ya tovuti. Kwa kubofya au kutembelea tovuti hii, unakubali ukusanyaji wa taarifa kwenye www.tiscontrol.com na zaidi kwa kutumia kuki. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye hati: Sera ya Faragha