Cheti na Hati

Tamko la Makubaliano la FCC au nembo ya FCC au alama ya FCC ni alama ya uthibitisho inayotolewa katika vifaa vya kielectroniki vinavyotengenezwa au kuuzwa ndani ya Marekani ikithibitisha ya kwamba muingiliano wa sumaku umeme (electromagnetic interference) kutoka kwenye kifaa upo chini ya kiwango kilichowekwa na Shirikisho la Tume ya Mawasiliano (Federal Communications Commission).

Nembo ya FCC inapatikana kwenye bidhaa hata zinazouzwa nje ya mipaka ya Marekani, kwa sababu ni bidhaa zinazotengenezwa ndani ya Marekani au zimesafirishwa kutoka Marekani, au zinauzwa pia ndani ya Marekani. Hili linafanya nembo ya FCC kutambulika duniani kote hata kwa watu ambao hata jina la Shirikisho la Tume ya Mawasiliano (Federal Communications Commission) hawalifahamu.


Alama ya CE ni alama kama inavyoonyeshwa juu katika ukurasa huu. Herufi za “CE” ni kifupisho cha maneno ya Kifaransa "Conformité Européene" ambayo yanamaanisha “Mapatano ya Ulaya”(“European Conformity”). Alama ya CE sasa inatumika katika nyaraka zote za EU.

Alama ya CE kwenye bidhaa ni tamko kutoka kwa watengenezaji wa bidhaa ya kwamba bidhaa imekidhi vigezo vyote muhimu vya sheria za Ulaya juu ya afya, usalama na za kuhifadhi mazingira.


Ufafanuzi na malengo ya agizo la RoHS ni rahisi kabisa. Agizo la RoHS linalenga kuzuia matumizi ya baadhi ya vitu hatari ambavyo huwa vinatumika mara kwa mara ndani ya vifaa vya kielektroniki. Kifaa chochote kinachotimiza agizo la RoHS kinapimwa kama kina madini ya Risasi (Pb), Cadmium (Cd), Mercury (Hg), Hexavalent chromium (Hex-Cr), Polybrominated biphenyls (PBB), and Polybrominated diphenyl ethers (PBDE). Kwa Cadmium and Hexavalent chromium, ni lazima ziwe chini ya 0.01% ya uzito wa kifaa. Kwa madini ya Risasi, PBB na PBDE, haitakiwi kuzidi 0.1% ya kifaa. Kifaa chochote kinachotimiza agizo la RoHS inabidi kiwe na 100 ppm au chini ya hapo ya mercury na pia mercury haitakiwi kuwa imewekwa ndani yake kwa makusudi. Ndani ya EU, baadhi ya vyombo vya kijeshi na vya afya huwa sio lazima kutimiza agizo hili la RoHS.


C-Tick ni utambulisho wa hati miliki iliyosajiliwa katika Mamlaka ya Vyombo vya Mawasiliano Australia “Australian Communications Media Authority”(ACMA). Alama ya C-Tick inaonyesha ya kwamba kifaa cha kielektroniki kilichowekewa kinatimiza agizo la mahitaji ya umeme nishati “electromagnetic compatibility (EMC)”. Alama ya C-Tick pia inatoa taarifa zinazoweza kufuatiliwa kati ya kifaa na msambazaji na pia ni sharti la Serikali ya Australia ili kuweza kuuza bidhaa kihalali ndani ya Australia.


Alama ya GOST-R ni alama ya utambulisho kwa vifaa vyote vya umeme vinavyosafirishwa kwenda Urusi. Sheria za Shirikisho la Urusi zinataka bidhaa zitimize na kufikia viwango vya usalama kulingana na viwango vya Urusi (GOST-R). Bidhaa isiyokuwa na alama ya GOST-R itakataliwa kuingia ndani pale itakapofika katika mipaka ya Shirikisho la Urusi.

Cheti cha GOST-R kinatolewa baada ya ukaguzi wa kitaalamu wa bidhaa kutoka kiwandani kwako ili kuhakikisha inafikia viwango vya usalama vilivyowekwa na sheria za Shirikisho la Urusi. Cheti cha GOST-R kitatumika ndani ya miaka mitatu na leseni ya kutumia alama ya GOST-R itakuwa halali kutumika kwa mwaka mmoja kisha itasajiliwa upya tena baada ya ukaguzi wa kiwanda mara moja kwa mwaka.


Utawala wa Haki za Uvumbuzi Nchini (The National Intellectual Property Administration) au kwa jina lingine Ofisi ya Hati China (Chinese Patent Office) ni ofisi ya hati kwa ajili ya watu wanaoishi nchini China.

ilifunguliwa mwaka 1980, kama Ofisi ya Hati kwa ajili ya Watu wa Jamuhuri ya China, kabla ya kubadilisha jina lake na kuwa State Intellectual Property Office (SIPO), na baada ya hapo kuwa National Intellectual Property Administration. Inahusika na kazi za hati na kuweka mipango ya mambo ya kimataifa katika kitengo cha haki za uvumbuzi (Intellectual property).

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK