DUKA-LA-KILA KITU, VYOTE CHINI YA PAA MOJA

Ukiwa na TIS, unapata kila kitu.

Tunatoa vifaa vyote vya Uangalizi wa majumbani vinavyokidhi mahitaji yako yote.

Tukiwa na zaidi ya vifaa 70 vya waya na visivyo na waya kwa ajili ya uangalizi wa nyumbani, tunatoa suluhisho lenye ubunifu na ambalo ni maridadi lakini kwa bei ya chini.

Tunatoa suluhisho la ubora wa hali ya juu kwa mahitaji yote ya uangalizi wa nyumbani ambalo linakidhi maisha ya kiwango chochote na jengo la aina yoyote. Kunavyozidi kuwa na ongezeko la uhitaji wa bidhaa zetu, inatubidi kukuza na kutanuka maeneo mengine ya dunia. Tunatangaza na kuuza bidhaa zetu kwa wasambazaji na wauzaji wetu.

Bidhaa za TIS na suluhisho:

TIS inazalisha vifaa vingi sana chini ya paa moja ili kukupa suluhisho kwa ajili ya taa zako, kiyoyozi, vifaa vinavyozunguka, uangalizi wa vifaa vya ndani, ulinzi, kuokoa pesa, kuokoa umeme, vihisio, saa, sauti video, uangalizi wa sehemu ya mapokezi hotelini, kupima umeme, kituo cha hali ya hewa, BMS, access control, intercom, umwagiliaji, kutoa tahadhali na programu pamoja na programu-tumizi.

Hii ni orodha ya baadhi ya bidhaa zetu tunazozitoa:

Teknolojia ya TIS ya waya kwa Uangalizi

Kutokana na mawasiliano ya "Advanced RS485", TIS-BUS hii ya njia-2inaendesha vifaa vingi vya TIS na kutoa amri, kuangalia na kuviendesha kwa wakati mmoja kwa kutumia mawasiliano ya njia-2 kwa kutumia waya wa data wa 4-Core Twist Pair ambao unapatikana sana sokoni.

TIS-BUS has gateways to AIR-BUS (Bidhaa zaTIS zisizo na waya) kwa kupitia AIR-BUS Convertor. Zinawasiliana pia kwa UDP/TCPkwa kupitiaTIS-IP-Port.

Topolojia?

Kwa kutumia teknolojia ya TIS-BUS,mfungaji anaweza kuunga mpaka vifaa 64 kwenye waya mmoja ambao unaweza kufika mpaka mita 1200 kwa urefu.

Kama mfungaji akiunganisha baadhi ya BUS loops kwa pamoja kwa kutumia madaraja ya mtandao (TIS-IP-PORT), basi mpaka vifaa 65280 vinaweza kuungwa kwa kila mtandao kirahisi kabisa.

TIS-BUS inaweza kuunganishwa kwa urahisi kabisa. Inatumia daisy chain, na inaweza kuwa wazi au imefungwa loop/ring au kuwa na topolojia ya nyota.

TIS-BUS Volteji ya Kutumika:

Injini ya TIS-BUS Engine inaweza kufanya kazi katika wigo mpana wa umeme kati ya volti 8-32. Na zaidi, ni nzuri kwa mazingira kwa sababu inachukua tu 15-32mA kwa vifaa vingi wakati vikifanya kazi. TIS-BUS inatumia nyaya 4 (jozi 2): jozi moja kwa ajili ya mawasiliano na nyingine kwa ajili ya umeme. TIS-BUS pia ina nyaya kadhaa kwa ajili ya usalama, ikiwemo usalama dhidi ya kugeuka kwa chaji (reverse polarity protection), usalama dhidi ya shoti, usalama umeme unapozidi, usalama dhidi ya joto na zaidi.

Teknolojia ya TIS isiyokuwa na waya kwa Uangalizi

Bidhaa za TIS-AIR vinatumia teknolojia ya WiFi ya 2.4 Ghz.Hivi vinatumia itifaki moja kama TIS-BUS, hivyo kuna wepesi mkubwa sana kuwasiliana kati ya vifaa vyenye waya na visivyo na waya.

Kila kifaa cha TIS Air kimetengenezwa na module ya WiFi ndani yake bila kuhitaji kiunganishi au kifaa kingine.

Kwa hatua 3 rahisi – funga, unganisha na uendeshe – unaweza kubadilisha swichi ya taa yoyote au thermostat au kuongeza vifaa vya kuendesha mapazia na vifaa vingine vya ndani au mfumo wa vipaza sauti ndani ya nyumba.

Kifaa cha kubadilishia AIR-BUS ni kifaa sahihi kwa ajili ya kubadilisha kifaa chochote kinachotumia waya ya TIS-BUS na kuwa kifaa kisichotumia waya yaani cha TIS-AIR.

Itifaki Wazi (Open Protocol):

Itifaki ya TIS-BUS yenye hatimiliki pia ni itifaki iliyo wazi inayotolewa kwa watengenezaji wataalamu na waunganishaji bila gharama yoyote. (Shirika lolote lililosajiliwa au mtengenezaji anaweza kwa urahisi na moja kwa moja akapata nyaraka zote za itifaki wanazohitaji baada ya kusaini makaratasi kadhaa ya mtandano.) TIS inahakikisha kuendelea kuwepo kwa teknolojia yetu ya uangalizi wa pekee kwa kuweka dhamana ya kwamba itaendelea kuwa wazi na kutumiwa na makampuni mengine na kufanya gunduzi ili kutumikia binadamu na mazingira.

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK