Mifano ya Kujifunzia

Kuna maelfu ya miradi ya kujiendesha ya TIS inayoleta furaha ya kipekee katika maisha ya watu mbalimbali duniani kote. Ifuatayo ni mifano ya kujifunzia, ikiwa ni pamoja na baadhi ya miradi yetu ya kujiendesha na bidhaa zetu janja za kibunifu.

Anti-Mold Sensor - TIS
Anti-Mold Sensor - TIS

Nyumba yenye Afya na Uendeshaji wa TIS

Baadhi ya watu wanaamini ya kwamba kukaa ndani nyumbani kuna matokeo bora zaidi kiafya kuliko kutoka nje katika miji mikubwa iliyojaa uchafuzi, lakini jambo hili sio kweli muda wote. Hewa ya ndani ya nyumba mara nyingine inaweza kuwa na athari hiyo pia kutokana na kushuka kwa ubora unaosababishwa na kemikali zenye madhara. Hii ni kwasababu maeneo yaliyofungwa yanasababisha kemikali zenye madhara kama vile carbon monoxide na Volatile Organic Compounds(VOCs), kukua zaidi ukilinganisha na maeneo yaliyo wazi.

Soma Zaidi
Smart hotel system – Energy saver – TIS

Uokoaji wa Umeme Katika Vyumba vya Wageni vya kisasa na TIS

Uangalizi wa matumizi ya umeme katika hoteli ni jambo lenye changamoto sana kwa wamiliki. Ukianza na kuweka joto linalotakiwa mpaka kuwasha taa kwa mwanga unaopendelewa, kuna uwezekano mkubwa wa wateja kurudi tena kukaa kwa mara nyingine kama wanakuwa na uwezo wa kurekebisha hali ya kwenye vyumba vyao ili viwe kama wanavyopendelea. Lakini, kuwapa uwezo wa kufanya hivi kwa kutumia teknolojia ya zamani kunapoteza umeme mwingi. Kwa mfano, kuna matatizo mengi yaliyopo juu ya mfumo wa zamani wa swichi za kadi.

Soma Zaidi
Smart hotel system – Energy saver – TIS
Green Mosque – sustainability - TIS
Green Mosque – sustainability - TIS

Uokoaji wa Umeme Kabambe ndani ya Misikiti na TIS Technology

Kila siku kuna swala 5 muhimu kwa Waislamu kumuomba mwenyezi Mungu, na Waislamu wengi wanakutana misikitini kwa ajili ya swala hizi. Kwa sababu ni nyumba ya Mungu, msikiti unatakiwa uwe na hali ya hewa safi na tayari kwa ajili ya swala. Lakini, kiuhalisia, kufanya hivi kunaweza kuwa na gharama kubwa kwenye bajeti ya msikiti na kwa mazingira kiujumla.

Misikiti mingi ina kiyoyozi cha ukutani kama mfumo wake mkubwa kiyoyozi, michache sana ina mfumo wa FCU. Kitu kimoja kinachofanana kati ya misikiti hii yote, mfumo wa kiyoyozi unakuwa unawaka kuanzia asubuhi mpaka jioni sana. Jambo hili linaonekana sana haswa katika maeneo yenye joto kama nchi za Ghuba, Afrika ya Kaskazini, India, na Kusini-Mashariki mwa Asia.

Soma Zaidi
Sustainability by TIS home automation

Je, Nyumba ya Ndoto Zako Inakula Umeme Mwingi Sana? Usijali, TIS inaweza kukusaidia.

Nyumba kubwa zenye vyumba vingi zinakula umeme mwingi sana. Familia na wageni wanaweza kusahau kuzima baadhi ya swichi za umeme. Pia, vyumba vya chini ya nyumba na vingine kama hivyo vinakula sana umeme hata kama hakuna mtu ndani yake.

Kiujumla, bili ya umeme itaongezeka kutokana na ukubwa wa nyumba yako.

Unaweza kudhibiti yote haya kwa kutumia mfumo wa kisasa wa uangalizi wa nyumba. Lakini, unaweza kuwa unajiuliza, je, ni rahisi kutumia mfumo kama huu? Je, unaweza kuokoa umeme? Je, ni kwa namna gani unaweza kuokoa umeme?

Soma Zaidi
Sustainability by TIS home automation
TIS Luna TFT panel installed in one of projects
TIS Luna TFT panel installed in one of projects

Kuta Zilizo Safi na TIS

Vidhibiti huwa kawaida vinawekwa katika ukuta pembeni ya milango, na hilo linafanyika katika swichi ya aina yoyote ya ukutani, iwe ni kwa ajili ya taa, thermostats, n.k

Idadi ya swichi za taa inatofautiana kwa kutegemea na ukubwa na utengenezaji wa jengo. Kwa mfano, nyumba ya starehe inahitaji taa nyingi sana. Sasa, fikiria jumla ya idadi ya swichi zitakazohitajika kwa ajili ya vipunguza mwanga vyote, FCU thermostat, floor heating thermostat, ceiling fan regulator, volume control, security console, curtain or shutter switches, na zaidi, na tuna ukuta uliojaa swichi kubwa na ndogo, jambo ambalo ni changamoto kwa mbunifu wa ndani yoyote. Wafungaji wanaweza kupata tabu pia, kwasababu mfumo wa kila kifaa unatabia yake na ukubwa wake, jambo linalofanya upangiliaji mzuri kuwa mgumu kuufanya.

Soma Zaidi
DALI64 project in Hilton Hotel – TIS Project reference

Nyaya chache, Udhibiti Zaidi katika Miradi ya Kibiashara na Mfumo wa Tis

Maeneo ya kibiashara kama majengo yenye maduka makubwa, migahawa na mahoteli zinatumia taa nyingi sana ili zing’ae na kuonekana za kuvutia. Pia, kwasababu ya masuala ya kiulinzi katika maeneo kama haya, hautakaa uone swichi ya ukutani ya taa hizo, kwasababu ni muhimu sana kila kitu kinachohusiana na taa kiwe kinadhibitiwa na msimamizi nyuma ya pazia.

Soma Zaidi
DALI64 project in Hilton Hotel – TIS Project reference
Smart street lighting automation by TIS in India
Smart street lighting automation by TIS in India

QUEENSWAY – Njia ya waenda kwa miguu ya kwanza ya Kujiendesha India

Inapatikana eneo la GIDA – barabara ya Chathiath, Queensway, ambayo ina muonekano mzuri pembezoni mwa ziwa, ni njia ya kwanza ya waenda kwa miguu ya kujiendesha yenyewe ndani ya India. Njia hii ya kimuziki ina urefu wa km 1.8, ikianzia kutoka kwenye barabara ya GIDA mpaka kwenye kanisa la Chathiath. Kwasababu njia ya miguu ya zamani haikuwa na upana wa kutosha, iliongezewa ndani ya ziwa na vipande vya mita 1 vya kujengea. Miti iliyokuwepo na soko la miti vyote vilizuiwa wakati wa ujenzi wa njia hii ya waenda kwa miguu. Njia hii imewekewa vigae vizuri kabisa. Huku ikiwa na mabenchi takribani 120 kwa ajili ya wageni, njia hii ni moja kati ya mambo mazuri ya kuyaona kwa kila mtu.

Soma Zaidi

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK