UJUMBE WA MKURUGENZI MTENDAJI

Wapendwa wateja,

Ningependa kuwasimulia moja ya kumbukumbu zangu nilipokuwa mtoto– kumbukumbu ambayo naamini ilikuwa nimoja ya masomo muhimu sana kwangu.

Nilipokuwa mdogo, sikupenda vile baba yangu alivyokuwa akizunguka ndani ya nyumba kama mlinzi kuangalia kama tumesahau kuzima taa sehemu Fulani ya nyumba. Ilikuwa nikama ndoto mbaya pale nilipojaribu kukimbia kucheza sebuleni na nikaacha taa za chumbani kwangu zinawaka. Hadi leo, huwa ninaisikia sauti ya baba yangu yakutisha na kuhisi uoga uliokuwa ukinipata mwilini huku nikisubiria kupewa adhabu.

Ninayo heshima kubwa sana kwa baba yangu, lakini nilikuwa nauoga na wasiwasi kuhusu kusahau kuzima kitu kila nilipokwenda, lakini taratibu, nilijifunza kuhifadhi umeme. Nakumbuka nilijisikia na kutaka kuzima kila kitu pale kilipokuwa hakitumiki. Ila taratibu, nilihisi hii yote ilitoka kwa baba yangu, na nilikuja kuwa mtu ambaye anapendelea kufundisha kitu hiki kwa familia yangu pia.

Kuwa makini nakutunza umeme kulinisaidia kugundua ya kwamba ukiachana na taa, kiyoyozi kwa kawaida kinakula umeme mwingi kuliko kifaa chochote cha umeme. Ugunduzi huu ulinisukuma kufanya ugunduzi wa mfumo wakuangali au meme. Nilifanya kazi sana ilikufikia ndoto yangu, na sasa TIS inayofuraha kukuletea vifaa vilivyona ufanisi wa hali ya juu vyenye uwezo wa kuokoa umeme kwa kiasi kikubwa kabisa. Vifaa vya kisasa vya kutumia majumbani ambavyo haviokoi umeme ni sawa na midolitu–kinakuwakinatumia rimoti lakini kinahitaji binadamu aweze kukiendesha. Mfumo elevu unaweza kufanya mambo mbali mbali katika midato fauti na unaweza kuokoa umeme moja kwa moja bila kuhitaji kuelekezwa na mtu.

Tena haswa ukiangalia namna watu wametingwa na kazi nyingi katika dunia yetu ya leo, kuwa na mlinzi makini kama alivyokuwa baba yangu inaweza kusaidia sana.

Umeme sio tu kwamba ndio unaendesha maisha yetu ya kil asiku, lakini pia ni injini inayoendesha uchumi na ndio unaonyesha mafanikio ya nchi duniani. Hiyo ndiyo sababu umeme, nitegemeo kubwa sana nasio kitu cha kupuuzia. Kama hatutunzi meme, tujue kuwa ni moja ya vitu vinavyoongeza ongezeko la joto duniani ambalo linachocheao ngezeko la vimbunga, mafuriko na majanga mengine yanayosumbua dunia nakugharimu mabilioni ya pesa serikali nyingi.

Kimsingi kabisa, maendeleo ya uchumi wetu na uhai wa mazingira yetu unategemea na tabia zetu pamoja na mambo tunayoyachagua. Sasa, fikiria kama kukiwepo na mfumo wa kisasa ambao unaweza kuokoa mpaka 50%ya matumizi ya umeme, chukua muda tu kufikiria ni kwanamna gani kutakuwa na mabadiliko makubwa kama kingetumika katika kila nyumba. Kifaa hiki kinafungua njia kwa matumizi ya vifaa vya kisasa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, sindio?

Kama wazalishaji wanaoongoza wa vifaa vya kuangalia majumba, TIS inatoa vifaa janja vya kisasa vyenye manufaa na vinavyofanya kazi kwa ajili ya kila aina yamtu na kila aina ya bajeti. Vifaa hivi vina saidia katika uangalizi wa taa, viyoyozi, mapazia, mota, vihisio(sensors), uangalizi wa vifaa vya sauti na video, vituo vya kutabili hali ya hewa, vipima umeme (energy meters),vifaa vya kumwagilia maji, saa, mifumo ya ulinzi, program nyingi za kompyuta na vitu vingine vingia mbavyo vyote vikiwa na lengo mojatu la kupunguza matumizi ya nishati na kuwa chini kadri inavyowezekana.

Mwisho kabisa napenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa baba yangu kwa kufanya jambo ambalo alikuwa akiamini ni sahihi na kwa kujali sana kizazi kilichokuwa mbele yake.

Ulikuwa mkarimu sana baba, na ninakushukuru kwa uliyoyafanya.

Turath Mazloum

MkurugenziMtendajinaMwanzilishi

TIS Control Limited

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK