Muda wa Kuwa Wajanja Kazini

Kadri teknolojia mpya zinavyozidi kuibuka, mahali pa kazi siku hizi panabadilika na kuwa salama zaidi, penye uzalishaji mkubwa zaidi, na penye mazingira mazuri. Ofisi za kisasa ni zaidi tu ya eneo la wazi lenye mwanga asili na samani chache; teknolojia janja inakwenda mbele zaidi ya hapo, inatengeneza njia mpya kabisa ya namna tunavyofanya kazi ofisini.

Ofisi janja ni ile ambayo sio tu watu lakini hata vifaa vya ndani yake vinafanya kazi kwa ufanisi. Ufanisi katika matumizi ya nishati, ulinzi, na mandhari mazuri ni vitu muhimu kwa ajili ya uzalishaji mzuri wa biashara. Kwa lugha nyingine, hivi ni vitu vinavyoifanya ofisi iliyo ya kijanja kufanikiwa zaidi.

Ni muhimu kuona namna ambavyo kujitegemea kukiwa pamoja na uhuru kunaweza kuongeza ubunifu na utendaji kazi wa wafanyakazi. Hebu fikiria mfanyakazi ambaye anakaa chini na kuandika ripoti ya uchambuzi wa onyesho lililopita huku mwanga wa chumba sio mzuri, haiwezekani kufungua dirisha, na akihangaika kupata “joto linalofaa” kwake na wafanyakazi wenzake.

solution smart office image

Taa za kijanja zinafaa sana katika mazingira ya ofisini, kwa sababu zinapunguza matumizi ya umeme kwa kiasi kikubwa. Sasa, ukiwa na vihisio vya TIS vyenye ufahamu, taa zitatumika tu pale mwendo unapogundulika ndani ya chumba. Kwa kutumia teknolojia ya kipimo cha wingi wa mwanga (lux meter technology) kiwango cha mwanga kitabadilishwa kulingana na mwanga wa jua uliopo. Na sio hayo tu. Wafanyakazi wanaweza kutazama na kubadilisha ukali wa mwanga na pia hata kubadilisha rangi ya mwanga katika vitovu janja (smart hubs).

Vihisio janja(smart sensors) vingi ni vifaa vya kugundua mwendo ndani ya nyumba ambavyo vinatumia infrared, ultrasonic, microwave, au teknolojia zingine kama hizo ili kugundua kama kuna mtu. Kwa kusafilisha taarifa hizo zilizokusanywa kwenda katika kifaa kingine janja, vihisio hivi vinaandaa mazingira ya kuwa na eneo la kazi linalotumia nishati kwa ufanisi. Vihisio hivi vinakuwepo ili kusaidia kusimamia kila kitu, kuanzia usimamizi wa joto ndani ya ofisi mpaka jagi janja la kutengenezea kahawa, litakalohakikisha kikombe cha kahawa kinakuwepo muda wote kinapohitajika.

Kihisio cha Afya kutoka TIS (TIS Health Sensor), kwa mfano, kinaweza kufungwa ndani ya vyumba vya maofisi ili kuhakikisha kuna mazingira ya afya nzuri kwa wafanyakazi ili waweze kuweka umakini wao katika kazi zao. Kifaa hiki janja kutoka TIS kinasaidia kurekebisha hewa ndani ya chumba ili wafanyakazi siku zote wafurahie kuvuta pumzi ya hewa safi, na katika chumba cha usimamizi watapokea taarifa ikiwa kuna kiwango kikubwa cha CO katika hewa ndani ya ofisi.

Mifumo janja ya TIS HVAC inafanya kazi kijanja kulingana na matumizi na joto la nje ili kurekebisha kiwango cha unyevu katika hewa ndani ya chumba.

solution smart office image

Chumba cha mikutano cha kijanja kinakua na vitu kadhaa ili kusaidia mikutano. Spika za darini kutoka TIS na motor za kunyanyua projector zitasaidia katika mchakato mzima.

Sasa, fikiria meneja ndani ya chumba cha mkutano akisema, “show the last season’s sale profits diagram on the screen”, na mifumo yote ikawaka yenyewe moja kwa moja. Hiyo ni ndoto ya baadhi ya wafanyakazi, na TIS technology itakusaidia kuona namna Amazon virtual assistant, Alexa anavyofanya kazi. Kifaa hiki kinamuwezesha mfanyakazi kufanya kazi zaidi ya moja kwa kutumia sauti yake tu kuendesha sehemu tofauti za mfumo moja kwa moja.

Usimamizi mzuri wa ulinzi ni matokeo mengine yanayoonekana katika sehemu za kazi za sasa. Kamera janja za TIS zinaweza kuona wigo mpana, hata mwanga unapokua ni mdogo, na zinaweza kusogeza picha kwa ukaribu sana. Zinakuwezesha kutazama eneo zaidi ya moja kwa wakati mmoja, kwa kugawanyisha skrini na kukuwezesha kuzifungua katika simu yako janja au kupitia kompyuta.

solution smart office image

Kumbuka, katika ofisi ya kijanja, kufanya maamuzi juu ya yale ya mfumo ni jambo unaloweza kulifanya, na vifaa vya kijanja vitakujulisha iwapo kuna jambo lolote la hatari linatokea.

Na mwisho, tukirudia kwa mara nyingine kusema kuwa faida zinazoweza kupatikana kwa kubadilisha mifumo ya kawaida katika sehemu ya kazi na kuweka mifumo janja ni kuwa na biashara yenye uzalishaji mzuri zaidi na rafiki kwa mazingira. Teknolojia janja ipoelekea, ni matarajio yetu teknolojia hii itatumika kufanya maeneo ya kazi kuwa bora na kuzalisha zaidi.

solution smart office image
solution smart office image
solution smart office image
solution smart office image
solution smart office image

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK