Hoteli na Menejimenti Mpya ya Kijanja

Soko la hoteli ni kubwa, na kupata njia ambayo inaokoa gharama katika kusimamia mamia na maelfu ya vyumba ni jambo la msingi iwapo kurekebisha hoteli ya kisasa ni jambo ambalo ni muhimu katika kuhakikisha mteja anaendelea kurudia kutumia huduma zetu katika ulimwengu huu wa kidigitali unaobadilika. Tukubaliane ya kwamba ni kazi ngumu sana kufunga chumba kimoja kimoja na vifaa vya teknolojia ya kisasa; ndiyo, ni rahisi kuwa na itifaki(protocol) moja muunganiko itakayosimamia sehemu mbalimbali ndogondogo za menejimenti ya hote. Na nyongeza ni kwamba, kubadili hoteli yako ya zamani na kuwa hoteli ya kijanja inakusaidia kukutangaza zaidi.

Shukrani kwa mfumo wa TIS Guest Room Management System (GRMS), taa za vyumba vya hoteli, viyoyozi, na vifaa vingine vinaweza kuunganishwa kwa kupitia mtandao janja na kutuma/kupokea data ili kuwezesha muunganiko kati ya BMS na GRMS, jambo lililo na umuhimu mkubwa katika kutoa usimamizi mzuri wa mzunguko wa hewa.

solution smart hotel image

Lakini ni Kwanini Teknolojia ya Chumba cha Kijanja ni Muhimu?

Urahisi na wakati mzuri katika hoteli kwa wateja ni jambo la kwanza linalokuwa akilini kwao. Wateja wanapenda kuwa na uwezo wa kupangilia vitu namna wanavyopenda binafsi; wanajisikia nyumbani zaidi kama watapata kile wanachokitaka. Kurekebisha joto la chumba na mwanga kwa kutumia tablet au kifaa kingine janja kinafanya wageni wajisikie kuwa na umiliki na kukaa kwa amani. Pia, kupata vitufe na swichi zote katika chumba kipya inaweza kuwa jambo gumu kidogo kwa wageni, hivyo kuwa na sehemu moja tu ambayo kwa kupangusa kidogo inawawezesha kusimamia na kubadilisha chochote ndani ya chumba ni jambo la msaada sana.

Ufanisi katika matumizi ya nishati ni jambo lingine. Wamiliki wa hoteli wanapendelea mifumo ya usimamizi iliyo rafiki kwa bajeti na iliyo endelevu. Ukiwa na teknolojia janja, vifaa vinatumika pale tu vinapohitajika. Kwa mfano, ukitumia kifaa janja kilichofungwa thermostat ndani yake kinasaidia katika kubadilisha joto la chumba chenyewe moja kwa moja kwa kuangalia hali ya hewa ya nje ya chumba, na inajizima kama chumba kitakuwa hakina mtu. Zaidi ya hayo, kihisio kinagundua pale mteja anapotoka chumbani na kinatuma taarifa hii kwenye swichi za taa na hivyo zinajizima zenyewe moja kwa moja. Hivyo, umeme mdogo unapotea, na biashara ya hoteli inakuwa ni rafiki zaidi kwa mazingira.

Nyongeza, chumba cha kijanja kinakusaidia katika nyanja zingine pia; katika hoteli zenye usimamizi wa zamani wa vyumba, mtu inabidi aende katika meza ya mapokezi au kutumia simu ili kuuliza taarifa au huduma fulani, lakini ukiwa na panel ya kijanja kunakusaidia hatua ya kutuma ombi/kujibu zaidi. Kwa kubonyeza kitufe kimoja tu, ombi la mteja la kupata huduma ya kufuliwa nguo litatekelezwa mara moja na meza ya huduma.

solution smart hotel image

Katika hoteli ya kijanja, timu ya menejiment wanaweza kufungua sehemu ya kusimamia wakiwa mahali popote. Hivyo, kufanya upangaji wa vyumba kwa ajili ya wageni kufanyika kwa urahisi na ufanisi zaidi; kiyoyozi cha chumba kinaweza kujiwasha moja kwa moja lisaa limoja kabla mgeni hajawasili, au taa za chumba zinaweza kupunguzwa mwanga ili chumba kiwe na mwanga unaofaa wakati mteja anawasili. Chumba janja cha mteja kinaweza kuwekewa mipangilio ya kukaribisha punde mgeni anapowasili.

Na nyongeza, wageni watafurahia zaidi viburudisho vya kuvutia ndani ya chumba. Mifumo ya kuburudisha ndani ya hoteli inawapa vipindi vya TV, filamu, na vingine vya kutazama ili kutengeneza kumbukumbu zisizosahaulika kwa wageni. Je, ni jambo gani ni bora zaidi ya kutazama episode ya Peaky Binders kwenye TV janja ambayo inajizima yenyewe punde unapopitiwa na usingizi, na kufanya iwe rahisi kuendelea palepale ulipoishia?

Hivyo kufanya iwe kazi ngumu kwa wageni wako kutoka kitandani. Katika hoteli ya kijanja, kila chumba kinaweza kufungwa na vifaa vya kugundua sauti. Kusimamia kwa kutumia sauti ni huduma kubwa inayoweza kutolewa na teknolojia ya vifaa janja. Wageni wataridhishwa na pale ambapo huduma za sauti zitakapowasaidia kuwasha au kuzima TV, taa na kiyoyozi.

Pia, badala ya kuwasiliana na mtu wa mapokezi ambaye muda mwingi amebanana pale wanapotaka kujua maeneo ya karibu ya kununua vitu au kula, wageni wako wanaweza tu kutumia msaidizi wa sauti kutafuta taarifa hizo kwa haraka zaidi, kwa kuwa ina maelfu ya tovuti ndani yake.

solution smart hotel image

TIS technology inatoa vihisio(sensors), paneli na vifaa suluhishi janja vya aina mbalimbali kwa ajili ya usimamiaji wa taa na joto. Sisi ni wanachama wa dhahabu wa Oracle Corporation na tunawezesha kushabihiana na programu za Opera, Fidelio, na Assa Aboly na pia vitasa vya Vingcard Zigbee. Pia inawezekana kuunganisha teknolojia ya TIS na Modbus, KNX, na itifaki zingine za BMS.

Kwa mara nyingine, tunarudia kusema kuwa fursa zinazotokana na kuwa na hoteli ya kijanja ni nyingi mno. Ifahamike kwamba kuwa tofauti ni muhimu sana katika kufanikiwa kwenye biashara ya hoteli, kama ukiweza kuifanya hoteli yako iwe tofauti kwa kuwa na teknolojia janja, moja kwa moja unaongeza idadi ya wateja watakaoridhika na huduma na kutengeneza njia ya kuwa na biashara yenye mafanikio zaidi huku ukisaidia kutekeleza sera ya kutumia nishati kwa ufanisi na kutengeneza kesho iliyo bora.

solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image
solution smart hotel image

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK