Uokoaji wa Umeme Katika Vyumba vya Wageni vya kisasa na TIS

Uangalizi wa matumizi ya umeme katika hoteli ni jambo lenye changamoto sana kwa wamiliki. Ukianza na kuweka joto linalotakiwa mpaka kuwasha taa kwa mwanga unaopendelewa, kuna uwezekano mkubwa wa wateja kurudi tena kukaa kwa mara nyingine kama wanakuwa na uwezo wa kurekebisha hali ya kwenye vyumba vyao ili viwe kama wanavyopendelea. Lakini, kuwapa uwezo wa kufanya hivi kwa kutumia teknolojia ya zamani kunapoteza umeme mwingi. Kwa mfano, kuna matatizo mengi yaliyopo juu ya mfumo wa zamani wa swichi za kadi. Wateja wanaweza kuweka kadi ya aina yoyote kwenye swichi, au wanaweza kuomba zaidi ya kadi moja. Hata kama mhudumu wa mapokezi akikataa kutoa zaidi ya kadi moja kwa mteja, anaweza kusema amepoteza kadi yake.

Teknolojia ya zamani ya kadi za swichi za hotelini

Kuna matumizi makubwa zaidi ya inavyohitajika ya taa na kiyoyozi kwa sababu ya vitu kuwa vimewashwa hata pale wageni wanapokuwa hawapo vyumbani, na hii inaweza kusababisha hasara kwa mmiliki. Ni kweli, hakuna mmiliki wa hoteli anataka kuwazuia wateja wake wasifanye kile kinachowafanya wakae kwa furaha, na pia wamiliki hawatarajii wateja wao waingie kwenye chumba cha baridi na giza. Hakuna mtu wa kulaumiwa. Wote wateja na wamiliki wa hoteli wana haki kutimiza yale wanayoyapendelea.

Baadhi ya wamiliki wa hoteli wanafikiria kwamba kama wakitenganisha kiyoyozi kutoka kwenye mfumo mkuu wa umeme, kutakuwa na upungufu wa matumizi ya umeme, wakati wengine wanafikiria kwamba kuweka vihisio vya mwendo (motion sensors) ndio suluhisho. Lakini, njia hizi zote zinashindwa kutatua tatizo. Kiyoyozi ndio kifaa kinachokula umeme kuliko vyote, na vihisio vya mwendo vinaweza kuwa tatizo kubwa sana kama vinafanya kazi kila vinapogundua mwendo, inamaanisha kwamba kiyoyozi na taa zinaweza kuzima ghafla wakati mgeni anasoma kitabu. Jambo la kutisha sana!

Kampuni ya vifaa vya uangalizi ya TIS inatoa suluhisho kwa vyumba vya wageni katika mahoteli kwa kutumia uvumbuzi wake wa kifaa cha kisasa cha kuwekwa juu kwenye dari: Energy Servant.

Kifaa chetu cha Energy Servant kinazidi mbali sana swichi za kadi za hotelini kwa uwezo wake wa kugundua uwepo wa binadamu ndani ya chumba. Kihisio hiki kinachofungwa juu kwenye dari kina vitu vingi vya kuchagua, ikiwemo PIR motion sensor, light harvest sensor, 2X digital inputs, infrared emitters inayoingiliana na aina zote za viyoyozi, TV brands infrared codes, temperature sensor, 24X flags and 32 lines of logic and timers.

TIS Energy servant, teknolojia mpya ya kuokoa umeme kwa mahoteli

Kwa kufunga kifaa hiki cha mlangoni kinachohisi katika mlango wa kuingilia, na kisha kukiunganisha na sehemu ya kuingizia taarifa za kidigitali za Energy Servant, na kisha kuweka programu kwenye logic lines, tatizo la kuwepo na kutokuwepo kwa mtu ndani ya chumba litakuwa limetatuliwa kabisa.

Zifuatazo ni mantiki (logic) zinazoweza kuwekwa kwa kihisio hiki ili kuweza kuangalia matumizi ya nishati bila kusumbua wageni:

Logic 1: Kama kuna mwendo wowote ndani ya chumba, kitawasha hali ya kuwa na wakazi.

Logic 2: Kama mlango mkuu utakuwa umefunguliwa na kufungwa, kiashiria kitawashwa kwa dakika moja ili kutazama mwendo ndani ya chumba. Kama hakuna mwendo utakaogundulika baada ya dakika moja, mfumo utawasha hali ya kuokoa umeme. Hii ni muhimu katika hali ambazo mgeni anaingia katika chumba kwa muda mfupi.

Katika hali ya kuokoa umeme taa zote zinakuwa zimezimwa kasoro taa za mwanga wa kulalia, ambazo zinawaka kwa masaa 3 tu ikiwa mgeni amelala. Pia, kiyoyozi hakitazimwa, lakini joto ndilo litakalopunguzwa kwa nyuzi joto 2. Hii itasaidia kuhifadhi nishati katika muda mrefu.

Logic 3: Kama hali ya kuokoa umeme ikiwa imewezeshwa na hakuna mwendo wowote utakaogundulika kwa zaidi ya masaa 3 – 5, taa za kulalia na kiyoyozi vitajizima vyenyewe. Inawezekana pia kuweka kiwango cha chini cha kiyoyozi.

Kama nyongeza, Energy Servant inaweza kuwasha na kuzima kiyoyozi kama ikigundua kwamba dirisha/mlango wa kwenye kibaraza uko wazi. Kitu pekee inachohitajika hapa ni kuweka viunganishi vya sumaku katika dirisha/mlango wa barazani na kuwekea programu ya maamuzi yanayohitajika kuchukuliwa.

Kihisio cha mwanga kinasaidia kutunza umeme kwa kuzima taa za barazani kama kuna mwanga asilia wa kutosha.

Mifumo ya kujiendesha ya TIS katika eneo la mapumziko ya Fairmount blue mountain huko Australia

Matumizi mengine yenye faida ya kihisio hiki ni thermostat iliyowekwa ndani yake, ambayo inasaidia kutunza joto linalofaa muda wote. Jambo hili ni la muhumu ili kutunza fanisi na vitu vingine vya ndani safi. Pia, katika maeneo yenye joto au kama chumba kitakuwa tupu kwa muda mrefu, unyevunyevu na harufu mbaya hautakuwa ni tatizo chumbani. Kihisio kimewekewa programu ya kuweza kubadilisha mfumo wa kiyoyozi na kuwa katika hali ya kukausha kama chumba kikiwa na joto linalozidi nyuzi 28 – 30C. Hii inaweza kufanyika mara kadhaa katika siku kama ikihitajika. Programu kama hii inaweza kuwekwa pia katika maeneo ambayo yana baridi kali ili kuzuia ukuaji wa fangasi.

Matumizi mengine ya kifaa hiki cha kisasa ni katika kuendesha TV. Kama hoteli inawapa wageni tablet ya chumba, anaweza kuitumia hiyo kubadilisha TV ya chumba.

Kihisio hiki kiliwekwa katika vyumba 20 ndani ya Fairmount Blue Mountain Hotel mjini Sydney. Matokeo yake ni kulikuwa na ongezeko la ubora katika uangalizi wa umeme na maono mengi chanya kutoka kwa wageni wengi ambao walifurahia mkao wao wa faragha katika hoteli hii.

Eneo la mapumziko la Fairmount blue mountain huko in Australia, Sydney – TIS

TIS inatoa nafasi kufikia mahitaji ya wamiliki wa hoteli pamoja na wateja kwa vifaa vichache tu na kwa njia ambayo itaokoa umeme kwa ufanisi mkubwa kadri iwezekanavyo.

Kwa taarifa zaidi au kupanga ahadi ya kuongea na washauri, wasiliana nasi kupitia www.tiscontrol.com.

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK