Nyaya chache, Udhibiti Zaidi katika Miradi ya Kibiashara na Mfumo wa Tis

Maeneo ya kibiashara kama majengo yenye maduka makubwa, migahawa na mahoteli zinatumia taa nyingi sana ili zing’ae na kuonekana za kuvutia. Pia, kwasababu ya masuala ya kiulinzi katika maeneo kama haya, hautakaa uone swichi ya ukutani ya taa hizo, kwasababu ni muhimu sana kila kitu kinachohusiana na taa kiwe kinadhibitiwa na msimamizi nyuma ya pazia.

Kwa mfano, eneo channel 180 za taa linahitaji angalau nyaya zenye 180 zenye moto na idadi ndogo kidogo ya nyaya zisizo na moto, huku kukiwa na vidhibiti vingi sana katika chumba cha uendeshaji.

Ulaji tofauti wa umeme ni jambo lingine la kuzingatia. Kudhibiti uzito kwa kutumia mfumo mmoja ni kazi ngumu, kama sio haiwezekani kabisa; baadhi ya taa zinahitaji kupunguzwa mwanga, wakati zingine huwa zinatoa mwanga wa rangi tofauti tofauti, na sio rahisi kupunguza mwanga kwa taa zenye ulaji wa umeme tofauti.

Tatizo lingine ni load voltage; baadhi ya taa zinafanya kazi kwa umeme mdogo wa takribani 12/24V DC, wakati zingine zinatumia umeme wa 110/220V AC.

Ukizingatia vitu vyote hivi, ni wazi kwamba mfumo wa kawaida wa uangaliaji au mfumo wa BMS hauwezi kupunguza mwanga kwa aina zote za mizigo hii iliyoungwa.

Kampuni ya TIS Smart Home inayo furaha kukuletea mfumo wa udhibiti wa aina zote za taa na itifaki za taa (lighting protocol systems) kwa kupitia vifaa vifuatavyo:

Mifumo ya TIS yenye waya na isiyo na waya ni suluhisho na inawezesha udhibiti wa mifumo yote iliyoelezewa hapo juu kwa kutumia mtandao mmoja. Pia, mfumo wa TIS unaweza kubeba zaidi ya vifaa 65,000 vyenye nyaya na visivyo na nyaya katika mtandao mmoja.

Ufungwaji wa mfumo wa kujiendesha wa TIS Automation DB katika Hoteli Hilton Hotel

Kwa utendaji kazi wake wa kipekee, mfumo wa TIS unaweza kukabiliana na matatizo ambayo itifaki(protocols) zingine zinakutana nayo kama vile DALI64, ambayo inaweza kubeba channel 64. Kwa kutumia mfumo wa TIS, namba hii inaweza kuongezwa na kuwa kubwa zaidi kwa kutumia controllers ambazo zinaweza kubeba channel 64 kila mojawapo. Na hivyo, unakuwa na udhibiti usiokuwa na kikomo juu ya taa kama ni kuzima/kuwashataa/kupunguza mwanga/rangi. Kwa taa zenye mzigo ambao hauwezi kubebwa na DALI drivers, TIS Relays na Dimmers ni vifaa vinavyoweza kutumika badala yake; jambo pekee unalotakiwa kufanya ni kufunga vifaa hivi pembeni mwa mzigo na kisha uvifunge kwenye mtandao wa waya wa TIS-BUS, hivyo tu.

Hoteli ya Hilton – Tanger Morocco- TIS GRMS

Vifaa vya TIS vilitumika katika Hoteli ya Hilton Tanger City Center na Makazi na pia Hilton Garden Inn Tanger City Center ili kuweza kudhibiti taa 180 ndani ya maeneo ya hoteli zao. Ufungaji wa nyaya ulipungua kwa 80%; TIS-DALI-64 Controller na TIS-BUS topology vilifanya ufungaji wa nyaya kuwa rahisi na wenye ufanisi zaidi. DALI ballast and light drivers zote zilifungwa pembeni ya mizigo, na waya wa data ulizungushwa kupitia vifaa vyote vya kisasa, pamoja na relays zingine na swichi za kupunguzia mwanga zingine.

Mfumo wa kusimamia taa wa TIS DALI ukifanya kazi ndani ya Hoteli ya Hiliton huko Morocco

Kwa kutumia panel moja ya Luna TFT iliyowekwa pembeni mapokezi, msimamizi anaweza kupunguza mwanga wa taa kwa 80%, 60%, 40%, na 20% ili kutengeneza hali ya mazingira tofauti kwa kubonyeza mara moja tu. Zaidi, TIS Logic Timer ilitumika kuendesha mazingira ya aina tofauti wakati wa mchana kwa kufanya mwanga wa ndani ufanane na mwanga wa nje.

TIS Luna panel katika mapokezi ndani ya Hoteli ya Hiltion huko Morocco
Skrini ya panel ya Luna – TIS Smart Hotel

Vilevile, TIS DALI na vifaa vya kupunguzia mwanga vilifungwa katika mapokezi, migahawa na vyumba vya mikutano vya miradi hii ya kibiashara ili kuweza kudhibiti aina tofauti ya mizigo kama vile LEDs na kuendelea.

Kampuni ya TIS Smart Home inafanya miradi migumu ya kufunga taa kuwa rahisi. Vifaa vyetu vinapunguza ugumu wa ufungaji nyaya na hivyo kutoa ufanyaji kazi bora ukilinganisha na vifaa vingine. VIfaa vya TIS sio tu kwamba vinafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu, lakini ni imara na muonekano wake ni wa kipekee na kuvutia pia.

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK