TIS website in Arabic now online

Jiskie uko Nyumbani.

Ili kuwa na tovuti yenye mafanikio, ni lazima kuweka juhudi zote katika kuifanya ionekane na kupatikana kwa watumiaji wa mtandao wengi kadri inavyowezekana. Kufanya hivi, ni muhimu sana kuwa na mahudhui ya lugha mbalimbali kwa ajili ya watumiaji.

TIS Automation Group inatoa huduma zake za mtandao kwa lugha kadhaa ikiwemo Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, n.k. ili kumrahisishia mtumiaji anapotembelea.

Hivi karibuni tafsiri ya Kiarabu imeongezwa katika sehemu ya kubadilishia lugha ya www.TIScontrol.com.

Hii imewekwa ili kuwawezesha watumiaji wa intaneti milioni 168 kutoka Uarabuni kuweza kutembelea tovuti kwa urahisi. Sasa watumiaji wetu wanaoongea lugha ya Kiarabu wanaweza kuelewa killa kitu, hawatakuwa wakibashiri tena taarifa zinazotolewa na watatumia muda wao mwingi kadri wanavyopenda kupitia bidhaa, taarifa, n.k mbalimbali zilizopo.

Nchi zinazoongea Kiarabu kama   Algeria, Bahrain, Chad, Comoros, Djibouti, Misri, Eritrea, Iraq, Jordan, Kuwait, Lebanon, Libya, Mauritania, Morocco, Oman, Palestine, Qatar, Saudi Arabia, Somalia, Sudan, Syria, Tanzania, Tunisia, Umoja wa Nchi za Kiarabu na Yemen sasa wanaweza kupitia tovuti kirahisi kupata mifumo ya nyumba ya kijanja kwenye tovuti ya kwanza ya aina yake kukamilika yenye lugha ya Kiarabu.

Mteja kwetu ni mfalme na tunaamini kwamba akiridhika itatutangaza zaidi, na itaongeza ufikiaji kwa watu wengi zaidi kwenye soko, itatusaidia kukua, na kuwa sehemu ya mapinduzi ya kirafiki yanayobadilisha mazingira yetu.

TIS Website News Image
TIS Website News Image

Tunatumia kuki kubinafsisha yaliyomo, kubinafsisha na kuchanganua utangazaji na kuhakikisha matumizi salama ya tovuti. Kwa kubofya au kutembelea tovuti hii, unakubali ukusanyaji wa taarifa kwenye www.tiscontrol.com na zaidi kwa kutumia kuki. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye hati: Sera ya Faragha

OK