TIS booth at CES Las Vegas exhibition

Ufahari Ukiunganishwa na Teknolojia; Panel ya Titania ni Bidhaa Mpya Elevu Kutoka TIS.

TIS Automation Group ilizindua toleo jipya la swichi za kijanja katika Onyesho la Watumiaji mjini Las Vegas, 2019. CES ni onyesho la kibiashara la kila mwaka lililoandaliwa na Shirikisho la Watumiaji wa Teknolojia (Consumer Technology Association) na linakuwa na maonyesho ya bidhaa na teknolojia mpya katika sekta ya elektroniki.

Washiriki walikutanishwa na Titania; kifaa kipya kutoka TIS cha kufungwa ukutani cha kugusa kinachoweza kusimamia ubora wa hewa, kutoa ripoti ya hali ya hewa, na matumizi ya umeme na kusaidia pia katika usimamizi wa taa, kiyoyozi, kivuli, mandhali, ulinzi na muziki. Swichi hii yenye muonekano wa kifahari ambayo inapatikana katika ukubwa wa kiwango cha Uingereza/Marekani ina Titania TFT, Titania 4G/3G, Titania Nurse Call panel, na Titania MUR, DND panel.

Ofisi za Makao Makuu ya TIS MAREKANI, Mfumo Elevu wa Texas, waliwasilisha suluhisho hili la kijanja kwa wageni ambao walitoka maeneo mbalimbali ya Marekani na nchi jirani. Kuhudhuria onyesho hili ilikuwa ni fursa ya kipekee kuwasiliana na wachora ramani za majengo, wabunifu wa ndani, wajenzi wa majengo, wauzaji, wasambazaji na wafungaji wa mifumo juu ya kukidhi kiu ya maarifa katika sekta ya nyumba za kijanja.

TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK