TIS is now official KNX manufacturer member

TIS Technology Sasa ni Chaguo Halisi la Urahisi Zaidi ya Ilivyowahi Kuwa

Ili kuendelea kuwa na thamani na jumuishi, wachukua maamuzi wa TIS Control wanafikiria namna za kibunifu na za ufanisi za kuunda bidhaa. Moja ya malengo makuu ya TIS group ni kusambaza vifaa suluhishi vya kijanja vinavyohitajika duniani kote katika idadi kubwa zaidi ya nchi. Kufanikiwa kwa hilo, wataalamu wa TIS waliamua kutoa nafasi ya kuunganisha itifaki(protocol) ya BUS na mtandao wa KNX.

KNX ni kiwango na ipo wazi kwa matumizi ya kujisimamia kibiashara na kwa majumbani ambayo inawezesha usimamiaji wa kiwango cha juu wa taa, viziba mwanga dirishani na shutters, HVAC, mifumo ya ulinzi, usimamiaji wa nishati, audio-video, skrini, usimamiaji kwa rimoti n.k. Viwango vitatu vya hapo mwanzo vilikuwa ni itifaki ya KNX:  Itifaki ya European Home Systems Protocol (EHS), BatiBUS, na European Installation Bus (EIB or Instabus), hivyo ni kiwango kinachotumika kimataifa haswa haswa Ulaya.

Kwa kuwa na KNX baadhi ya mawasiliano ya moja kwa moja ya media ikiwemo nyaya zilizofungama pamoja (twisted-pair wiring), power line networking, radio frequency, infrared, na Ethernet vimewezeshwa ndani ya TIS smart home; hii inamaanisha uwezo wa kusimamia zaidi ndani ya nyumba.

Weka mipangilio yako ya M/MI/S Group ndani ya programu ya ETS ili kufanana na id na namba ya kifaa chochote cha Subnet katika TIS dimmers au Relays. Au weka mipangilio katika panel yoyote ya TIS kutuma anuani ya kundi la KNX kwenda kwenye actuator yoyote ya TIS.

Sasa kwa urandanaji wa KNX, mfumo janja wa TIS unapendekezwa kwa kiwango cha juu kwa sababu unaingiliana na mradi wowote na ni rahisi kutumia.

TIS Website News Image

Tunatumia kuki kubinafsisha yaliyomo, kubinafsisha na kuchanganua utangazaji na kuhakikisha matumizi salama ya tovuti. Kwa kubofya au kutembelea tovuti hii, unakubali ukusanyaji wa taarifa kwenye www.tiscontrol.com na zaidi kwa kutumia kuki. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye hati: Sera ya Faragha

OK