TIS's integration with Siri in all iPhone IOS applications

Usimamizi wa Kijanja Ulioboreshwa katika Jengo la Aina Yoyote

Teknolojia ya kijanja inaendelea kukua kila siku. Waunganishaji na wabunifu wa vifaa hufikiria namna mbalimbali za kuboresha majengo elevu (intelligent buildings).

Kuna wasaidizi kadhaa wasio bayana (virtual assistants) unaweza kuwapata kwenye soko wanaoweza kukusaidia kufanya mambo. Mojawapo ni, Siri, msaidizi asiye bayana anaepatikana katika bidhaa za Apple ambaye unaweza kumuuliza maswali na akatoa majibu, akatoa mapendekezo, na kuwasiliana na huduma mbalimbali katika intaneti, kama vile Worfram Alpha, Yelp na Trip Advisor.

Huduma hizi sasa zinapatikana kwa watumiaji wa TIS technology; bodi ya mameneja wa kampuni ya TIS imesaini mkataba wa ushirika na watendaji wa Apple. Wateja wetu sasa wanaweza kuwa na mtandao janja zaidi unaoweza kutafuta, kupokea maelekezo ya sauti, na mapendeleo ya mtumiaji katika kusimamia vifaa janja.

Tunaongeza uwezo wa kushirikiana na vifaa vingine kwa kuruhusu app zingine kuweza tumika pamoja ili huduma ziweze kupatikana kwa kila mtu. Sasa kwa wapenzi wa iOS wanaweza kufurahia teknolojia ya TIS kama vile kwa watumiaji wa Android pia. Ukiwa na vifaa suluhishi kutoka TIS vilivyowezeshwa na kutumika na Siri, unaweza kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi wa maandishi huku ukiwa unaendesha gari, au unapokuwa mikono yako yote inatumika, au tu ukiwa na haraka. Muulize Siri akupe ripoti ya hali ya hewa kwa kutumia TIS Luna panel au 4-T sensor.

Unaweza kuwasiliana kirahisi kabisa; uliza tu unachokitaka na sisi tutafanya kwa niaba yako.

TIS Website News Image

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK