TIS AIR new smart home technology based on WIFI

Vumbuzi Zinazofanya Kazi katika Maeneo ya Kijanja; Teknolojia ya TIS AIR

Ongezeko la idadi ya watu na mabadiliko makubwa katika teknolojia vimeteleta athari kubwa katika miji mingi duniani kote. Matumizi ya nishati yameongezeka sana na maamuzi makubwa inabidi yafanyike ili jamii iweze kukua. Kwa sababu teknolojia ya kidigitali ni moja ya vitu muhimu katika matumizi ya kila siku ya kijamii, kutengeneza vifaa vinavyopunguza matumizi ya nishati na kurahisisha maisha ni jambo lenye umuhimu mno. Ili kuboresha ubora wa maisha na kuongeza usalama kwa wote, TIS Automation Group imeleta kwenu wireless solutions.

Duniani kote, vifaa suluhishi visivyotumia waya (wireless solutions) kutoka TIS vilivyowezeshwa na IoT, vinatumika katika miji mbalimbali kuisaidia kuwa endelevu, salama, na rahisi kuishi ndani yake. Smart air panels, sensors, bidhaa za A/V, n.k. vinaletwa sokoni ili kuhudumia watu wanaoishi katika ulimwengu wa sasa wa kuwa na ufanisi katika matumizi ya nishati. Kufunga air solution katika nyumba ni rahisi sana; kitu kinachohitajika ni mtandao wa Wi-Fi tu. Mtumiaji anaweza kusimamia kila kitu kwa urahisi akiwa sehemu yoyote kwa kutumia simu yake ya mkononi tu. 

Teknolojia ya TIS AIR inafanya kila kitu kuwa na muunganiko; sio tu kompyuta na simu janja, bali kila kitu: saa, spika, taa, kengere za mlangoni, kamera, madirisha, viziba mwanga madirishani, vichemshia maji, vifaa vya ndani, vifaa vya kupikia n.k. Vifaa vyote hivi vinaweza kufanya kazi na itifaki (protocol) ya TIS-AIR, kukutumia taarifa, na kisha kuchukua amri yako.

Mji wa kijanja uliojengwa na nyumba za kujanja nicho kitu pekee kinachohitajika ili kuwa na mfumo rafiki kwa mazingira wa kijani, endelevu na wenye ufanisi katika matumizi ya nishati.

TIS Website News Image

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK