TIS's integration with Cool Automation for VRF Air condition control

Piga Hatua Inayofuata Mbele Ukiwa na Usimamizi Unganishi wa TIS na CoolAutomation

TIS na CoolAutomation wanayo furaha kutangaza muingiliano wa hali ya juu wa vifaa vya kusimamia joto katika miradi ya nyumba janja ifuatao.

CoolAutomation ni kampuni ya kibunifu yenye maelfu ya wateja na wasambazaji wanaopatikana katika nchi zaidi ya 90. Vifaa vya kampuni hii vinafanya kazi kwa kutegemea teknolojia ya IoT(Internet of Things), kuwezesha IoC, nadharia mama ya mifumo ya usimamizi wa hali ya hewa. Sasa kwa kuwa TIS & CoolAutomation wameungana nguvu katika kutoa vifaa suluhishi, unavyoweza kuvifanya na mifumo ya VRF & HVAC ni vingi sana katika aina yoyote ya mradi iwe ni katika makazi ya kuishi, katika biashara au katika mradi wa kiwandani.

Hivi karibuni vifaa vingi vyenye uwezo wa kusimamia matumizi ya nishati vimetengenezwa kuepusha kutofautiana kwa thermostat (thermostat wars) na mipangilio itakayopelekea kupanda na kushuka kwa joto na hivyo kufanya kila kitu kuwa rahisi. Vifaa vya TIS sasa vinaweza kufanya vitu vingi zaidi ya hapo kabla, thermostat ambazo zinaweza kujiendesha na pia kupokea maelekezo (programmable) kwa ajili ya kusimamia hali ya joto pamoja na unyevu.

Fanya mazingira yanayokuzunguka yawe mazuri na salama kukaa kwa kutumia mifumo yetu ya HVAC ambayo inaweza kusimamia sehemu tofauti katika eneo moja, kama vile mfumo wa VRF kutoka Daikin, Samsung, LG, York, TRANE, Hitachi , Mitsubishi, oGeneral na zaidi. Vifaa jumuishi kutoka TIS + CoolAutomation vinasaidia kudhibiti joto lisibadilike, kupunguza kwa kiasi kikubwa bili ya umeme, na kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kupunguza nyayo za kaboni. Fanya vyumba vya watoto, sebuleni, kliniki, ofisi n.k. viwe na hali ya mustarehe kukaa.

TIS Website News Image

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK