India Kusini (Aprili.2014) – Watengenezaji wa vitovu elevu vya kusimamia (control hub) hivi sasa wanajaribu kuboresha vifaa vilivyowezeshwa na IT katika ngazi zote za uzalishaji, ufanisi katika matumizi ya nishati, na urahisi. Hii inafafanua ni kwanini kila mahali watu wanatumia vifaa hivi janja vya mageuzi vya majumbani. TIS Automation Group, mzalishaji kiongozi wa vifaa vya kijanja alifanya semina India Kusini, ambayo ilifafanua zaidi teknolojia iliyo nyuma ya bidhaa janja zinazouzwa na kazi zake zinazofanya ziwe na ufanisi mkubwa katika kutumia nishati. Afisa Mtendaji Mkuu wa TIS, Turath Mazloum, pia alifafanua juu ya uvumbuzi mpya wa teknolojia ya TIS BUS/AIR. Teknolojia janja ya TIS sasa inaweza kufanya kazi pamoja na aina zote za miradi iwe ni ya wiya (wired) au isiyo na waya (wireless) ndani ya India Kusini.
Malengo makuu ya tukio hili lilikua ni kuwatambulisha wasikilizaji juu ya mtandao wa TIS na bidhaa suluhishi pamoja na kutoa hotuba na dondoo za kuboresha zaidi biashara.
Wahudhuriaji waliovutiwa walijisajili kwanza kupata kozi katika fomu ya maombi inayopatikana hapa https://www.tiscontrol.com/tptis/En/ad_training.html. Katika mafunzo ya siku-tatu katika kituo cha mafunzo kilichopo India Kusini, Turath Mazloum alifundisha zaidi ya washiriki 30 juu ya itifaki (protocol) ya TIS na kuweka maelekezo (programming) kwa kutumia mfululizo wa mafunzo ya kazini, na programu za bespoke. Kozi hizi zilikuwa zimefungamana na sera ya TIS ya kukua na kufundisha wanafunzi wenye vipaji waliovutiwa, wanaotaka kuwa bora katika teknolojia janja na BMS. Mwisho wa siku, washiriki waliandaliwa kupokea cheti rasmi kutoka TIS ambacho kinawawezesha kushirikiana na wauzaji mbalimbali na wawakilishi wa TIS.
Tunatumia kuki kubinafsisha yaliyomo, kubinafsisha na kuchanganua utangazaji na kuhakikisha matumizi salama ya tovuti. Kwa kubofya au kutembelea tovuti hii, unakubali ukusanyaji wa taarifa kwenye www.tiscontrol.com na zaidi kwa kutumia kuki. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye hati: Sera ya Faragha