TIS dealer participated in HIA expo in Sydney, Australia

Tulipotembelea mji wa Sydney katika jengo na maonyesho ya kipekee, TIS ilizindua vifaa vyake vyenye muundo mpya vya kusimamia taa/kiyoyozi.

DH & S Automation Group, wawakilishi wetu mjini Sydney, waliongoza banda la maonyesho na kuonyesha moduli mpya za TIS ambazo ni TE Dimmer na HVAC katika maonyesho ya HIA ambapo vifaa bora kutoka pande zote za dunia vinaonyeshwa na matoleo mapya yanazinduliwa. Onyesho hili lilikua ni jukwaa zuri sana kwa wasambazaji wengi, watengenezaji wa vifaa vya kidigitali na wauzaji wa kimataifa kuungana na kujadili vumbuzi mpya katika soko la teknolojia za kijanja.

Wataalamu wetu waliwasilisha vifaa janja viwili suluhishi kwa matumizi ya nyumbani vyenye ufanisi mkubwa na ustahimilivu. Trailing Edge (TE) Dimmer ni kifaa janja ambacho ni suluhisho kwa ajili ya kupunguza mwanga wa taa katika nyumba yoyote au mradi wa kibiashara. Moduli hii inapatikana ikiwa na channel 2/4, inaweza kutumika kupunguza taa za volt kubwa pia. Hata hivyo, inaweza kuunganishwa na vifaa vingine janja katika mradi wa mteja kwa sababu inaweza kufanya kazi na mfumo wa TIS-BUS.

HVAC Module ni kifaa kingine suluhishi kilichotambulishwa kwa watu katika onyesho hili kubwa. Moduli hii imetengenezwa maalumu kwa ajili ya kusimamia vipunguza mwanga (dimmers) vya HVAC na VAV, pamoja na kiyoyozi cha mfereji (ducked split), AHU, Air Handling Unit, na VRV0-10V. Inaweza kutumika pamoja na Luna panel, moja kati ya paneli janja ya ukutani kutoka TIS maarufu zaidi, kwa kutumia kihisio chake cha nje cha joto. Moja ya sifa za moduli hii ni uwezo wa kuonyesha ripoti ya matumizi ya umeme pamoja na uwezo wa kujiendesha yenyewe. Kuondoa unyevu katika eneo sehemu yenye hali ya hewa ya unyevu ni rahisi sana unapokuwa na module janja ya BUS.

Wageni kutoka Sydney na miji mingine ya Australia kama vile Melbourne,   Brisbane, Perth, Adelaide, Gold Coast, Canberra na Newcastle walitembelea banda la TIS

Ilikuwa ni jambo la kipekee kwa timu nzima ya TIS kushiriki katika maonyesho haya kwani ilitoa fursa ya kufanya majadiliano na wageni juu ya umuhimu wa vumbuzi za kiteknolojia na zinazookoa nishati zilizopo ndani ya TE Dimmer/HVAC module.

TIS Website News Image
TIS Website News Image

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK