QUEENSWAY – Njia ya waenda kwa miguu ya kwanza ya Kujiendesha India

Inapatikana eneo la GIDA – barabara ya Chathiath, Queensway, ambayo ina muonekano mzuri pembezoni mwa ziwa, ni njia ya kwanza ya waenda kwa miguu ya kujiendesha yenyewe ndani ya India. Njia hii ya kimuziki ina urefu wa km 1.8, ikianzia kutoka kwenye barabara ya GIDA mpaka kwenye kanisa la Chathiath. Kwasababu njia ya miguu ya zamani haikuwa na upana wa kutosha, iliongezewa ndani ya ziwa na vipande vya mita 1 vya kujengea. Miti iliyokuwepo na soko la miti vyote vilizuiwa wakati wa ujenzi wa njia hii ya waenda kwa miguu. Njia hii imewekewa vigae vizuri kabisa. Huku ikiwa na mabenchi takribani 120 kwa ajili ya wageni, njia hii ni moja kati ya mambo mazuri ya kuyaona kwa kila mtu.

Mpangilio wa LED katika njia hii inafanya iwe ni kivutio cha kipekee pembeni mwa ziwa. Pamoja na chuma ya pembeni na mandhari mazuri pembezoni mwa barabara, ni jambo la kuvutia na kupendeza kuwa katika njia hii. Njia hii pia ina ukumbi mkubwa wa kuweza kubeba watu 50.

Mji wa Kisasa na TIS, Mtaa unaojiendesha

Kamera za CCTV zimefungwa katika njia hii, ambazo zinajiendesha kwa kutumia teknolojia ya TIS. Ta azote zinaendeshwa na TIS Relays na zimewekwa kuwaka kabla jua halijazama na kujizima katika mida maalumu kwa kutumia Automation Timer Module kutoka TIS. Na zaidi, TIS Audio Matrix itacheza muziki bila mpangilio kutoka kwenye vituo vya redio mbalimbali na kuweka orodha ya muziki kila siku. Mfumo mzima unaweza kuendeshwa kwa kutumia simu ya mkononi ya kisasa. Njia hii itakuja kuwa jambo la kwanza la kipekee kuwahi kuwepo, na vitu vyote vitakuja kuwa wazi kwa umma.

Taa za mtaa wa kisasa zinazojiendesha na TIS huko India

MALENGO YALIYOFIKIWA

  • Uokozi wa umeme na pesa kwa kuunganisha uchambuzi wa kimantiki(logical analysis) na utoaji wa taarifa huku ikiwa rahisi kabisa kudhibiti.
  • Kuboresha matumizi ya umeme kwa kutumia mikakati ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja.
  • Kupunguza ongezeko la utoaji wa kaboni.
  • Kuzuia matumizi ya taa mpaka tu kwa mida ambayo zinahitajika ili kuokoa umeme na kuwa na matumizi bora.
  • Kuondoa upotevu wa umeme.
  • Kuzima/kuwasha na kupungua kwa mwanga wa taa wenyewe kwa kujitegemea katika njia hii ili kurahisisha udhibiti na utumiaji kwa ratiba ya kila siku.
  • Kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa kwasababu ya utumiaji bora wa umeme.
  • Inawezekana kubadilishwa muda wowote ili kutimiza mahitaji yanayobadilika muda na muda.
TIS Kerlay , Kothin , Uendeshaji wa Taa na Muziki katika Mtaa wa Kisasa

Hatua ya pili ya mradi ni kuongeza grills mbili pembezoni mwa barabara, vyoo viwili, kamera za kisasa za CCTV zinazoweza kuona usiku, na WiFi ya bure, ambavyo vitakuwa vinapatikana ndani ya miezi miwili.

Mradi huu unaonyesha Teknolojia za TIS haziishii tu katika uangalizi wa ndani ya majumba yetu; tunaweza kuongeza vifaa vya udhibiti na uangalizi katika mradi wowote.

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK